KAZI ZILIZOFANYIKA KWA ROBO YA PILI YA MWAKA 2016/2017.
Tokeo tarajiwa 1:
Kujenga uwezo kwa Serikali za Mitaa juu ya kuweka Vipaumbele vya Maliasili katika Mipango ya Bajeti kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya.
Kujenga uwezo kwa timu ya uwezeshaji ya wilaya jinsi ya mtiririko wa utoaji wa taarifa
Tokeo tarajiwa 2:
Kuboresha utawala bora na usimamizi endelevu wa maliasili kupitia kamati za usimamizi za vijiji na watumiaji wakuu wa rasilimali hizo katika ngazi ya kijiji
Kujenga uwezo na utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji kwa kuboresha utawala bora na usimamizi endelevu wa maliasili ikiwa ni pamoja na kuwezesha mpango wa matumizi bora ya ardhi wa vijiji
Kuunda kamati ya matumizi bora ya ardhi katika kila kijiji (VLUM), katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama na Kabare
Kutoa mafunzo kwa kamati ya matumizi bora ya ardhi juu ya hatua za kufuata wakati wa kuandaa matumizi bora ya ardhi, katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama na Kabare
Kufanya utambuzi wa mipaka ya vijiji/kujua mipaka ya kijiji chao ,eneo la ardhi yao ya kijiji na kujua matumizi ya ardhi yao kwa sasa, katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, na Churazo
Kuijengea uwezo timu ya wawezeshaji wa Mpango shirikishi wa jamii wa msitu (PFM) juu ya hatua sita za kuandaa mpango shirikishi jamii wa msitu
Kuhuisha/kuunda kamati za Maliasili za vijiji katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama na Kabare
Kufanya mafunzo kwa kamati za Maliasili juu ya majukumu na wajibu, Sera na Sheria zinazohusiana na Maliasili, katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama na Kabare
Tokeo tarajiwa 3:
Watumiaji wakuu wa maliasili,wachakataji wa mazao ya maliasili,na wafanayabaishara wa maliasili wafanye shughuli za maliasili kwa faida na kwa uendelevu
Kutambua na kuainisha vikundi vya kuweka na kukopa na vikundi vya kijamii vilivyopo katika maeneo ya mradi, katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama na Kabare
Kufanya ziara za kuwajengea uwezo/mfunzo VICOBA,SACCOS na vikundi vya kijamii, vijiji vya Kazilamihunda na Juhudi
Tokeo tarajiwa 4:
Kuimarisha uwezo wa kitaasisi na uwajibikaji wa wadau muhimu kwa ajili ya kuboresha ushiriki wa jinsia,utawala bora, uratibu wa Ukanda (landscape), na utekelezaji wa usimamizi shirikishi wa maliasili
Kutambulisha mradi katika ngazi ya kijiji (mkutano wa hadhara) na ngazi ya kata (Baraza la maendeleo la kata-WDC), katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama na Kabare
Kuanzisha na kuziwezesha klabu za mazingira kwenye shule za msingi (7) na sekondari (3,) katika vijiji vya Rumashi, Nyabibuye, Churazo, Gwarama, Kabare, Kazilamihunda na Juhudi
Wafanyakazi wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya walipanda miti kwenye vyanzo vya mbizi na Kabare siku ya kupanda miti kitaifa ili kutunza vyanzo vyetu vya maji.
Watendaji wa kata na watendaji wa Vijiji walihimizwa kusimamia zoezi la upandaji miti kwenye vyanzo vya maji katika maeneo yao ili kuweza kulinda na kutunza mazingira na vyanzo vyetu vya maji.
Tumeweza kuwadhibiti na kupambana na wanyama waharibifu katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ya moyowosi.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KIPINDI CHA ROBO YA PILI YA MWAKA 2016/2017 KITENGO YA ARDHI KAKONKO
1.1 Utangulizi
Idara ya Ardhi Wilayani Kakonko inatekeleza majukumu yake kulingana na Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999, Sheria ya Upimaji na Ramani ya mwaka 1957 na Sheria ya Mipangomiji Na. 8 ya mwaka 2007. Sheria hizo zinatekelezwa sambamba na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Na. 7 ya mwaka 1982 na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya mwaka 1982 na Kanuni za Upangaji Viwango vya Upimaji Mjini za mwaka 2011.
Ifuatayo sasa ni taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Kitengo cha Ardhi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016/2017.
1.2 Upimaji wa viwanja.
Kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016/2017 Kitengo cha Ardhi kimefanikiwa kupima viwanja vifuatavyo:
Viwanja 125 ambavyo vimewekwa alama na majira nukta (Dermacation na coordination) kazi ya kupanda mawe ya upimaji(beacons) inaendelea kwa maeneo yasiyokuwa na marekebisho ya kitaalam ili kuweza kuchora ramani ya Upimaji (Survey Plan) kwa ajili ya kupeleka Wizara ya Ardhi kuidhinishwa na mkurugenzi wa Upimaji na Ramani.
1.3 Uandaaji wa Hatimilki.
Kitengo cha Ardhi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016/2017 kimezidi kuandaa hati kwa wananchi na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na hati miliki.
1.4 Ukaguzi wa ujenzi.
Katika kipindi cha robo ya pili iliyopita, kitengo cha Ardhi kimefanya ukaguzi katika maeneo ya Kakonko Mjini kwa ajili ya kudhibiti ujenzi holela katika maeneo hayo. Aidha katika kipindi hicho, wadau mbalimbali wa ujenzi walihamasishwa kuwasilisha ramani za nyumba walizotazamia kujenga ili wapatiwe vibali vya ujenzi. Hii ni katika kutekeleza Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007 kifungu cha 29 ambacho kinazuia maendelezo yoyote ya ardhi kufanywa bila kuwa na idhini na kibali cha ujenzi.
1.5 Migogoro ya Ardhi.
Migogoro ya ardhi imekua ikitokea baina ya mtu na mtu, kijiji na kijiji, migogoro baina ya mtu na mtu ofisi ya ardhi imekua ikijaribu kutoa ushauri wa kitaalam ili kuleta maridhiano baina ya pande mbili,
Pia migogoro ya Kijiji na Kijiji imekua ikiibuka kwa vijiji ambavyo vimegawanyika na kuzaa vijiji vipya,Mfano uliokuwa Mgogoro wa Kijiji cha Kabare na Luhuru, ufumbuzi wa mgogoro huo ni kutokana na sharia ya Ardhi No 4 na No 5 ya mwaka 1999 kila raia anahaki ya kufanya shughuli popote ndani ya nchi ya Tanzania,kwahiyo basi Mgogoro huu suluhisho lake limepatikana kwa Vijiji vyote viwili kuridhia mpaka wa kutenganisha vijiji hivyo bila kuadhiri shughuri zate zilizokuwa zinafanywa kwa pande zote mbili na utaratibu wa kuvipima vijiji hivyo utafuata kwa kushirikisha pande zote mbili.
Mgogoro wa mashamba kati ya wananchi wa Kijiji cha Kiga na Nyakayenzi nao suluhu imepatikana kwa kutumia ibara ya 24(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na bila kuathiri vifungu vifungu vingine vya sheria za ardhi kila mtu anaruhusiwa na anayo haki ya ulinzi wa mali yake kwa mujibu wa sheria.
Ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Umma (kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 na sheria ya ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999) kila Mtanzania anayo haki ya kumiliki na kutumia ardhi popote pale ndani ya mipaka ya Tanzania kwa mujibu wa sheria, kwahiyo basi kila mwananchi aliyekuwa akimiliki na kulima mashamba kwenye bonde la mto Ruhwiti kabla ya mipaka ya vijiji vya Nyakayenzi na Kiga kuwekwa, ataendelea kumiliki na kulima katika eneo hilo bila kujali eneo hilo lipo katika Ardhi ya kijiji cha Nyakayenzi au Kiga. Kwa maana hiyo Wananchi wa Kijiji cha Kiga waliokuwa wanamiliki na kulima mashamba katika eneo la mto Ruhwiti kabla ya mipaka kuwekwa wataendelea kulima katika eneo hilo. Aidha Kijiji chochote kinachohitaji kurejeshewa maeneo/ Ardhi hiyo inayomilikiwa na kutumiwa na wananchi wa kijiji kingine wanajibika kufuata taratibu na sharia za kurejeshewa maeneo / Ardhi yao ikiwa ni pamoja na kulipa fidia wale wote waliokuwa wanamiliki mashamba kwenye maeneo hayo baada ya wataalam kutoka ngazi ya halmashauri kutathmini maeneo hayo na si vinginevyo.
Hivyo basi ni wajibu wa kila Halmashauri ya Kijiji husika na wananchi wake kuzingatia maamuzi na makubaliano yaliyofikiwa ili shughuli zote za maendeleo ziweze kufanyika pasi kuendeleza migogoro isiyo na tija.
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: 028-2820137
Simu ya Mkononi: 0757470800
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa