Miundombinu ya Umwagiliaji
Wilaya ya Kakonko ina jumla ya skimu 6 za umwagiliaji maji mashambani na mabwawa 2 kwa ajili ya matumizi ya maji ya nyumbani na mifugo. Kati ya skimu hizo, skimu 5 zinazalisha vizuri wakati skimu ya Nyaronga katika Kijiji cha Nyamtukuza inazalisha kidogo kutokana na kuwa ujenzi wa miundombinu umekamilika hivi karibuni. Katika skimu hizo kuna jumla ya Ha. 1,756.5 zilizopimwa ambapo jumla ya Ha. 1,194 (68%) zinalimwa na jumla ya wakulima 2,568. Wilaya ina mpango endelevu wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji ambapo imekamilisha mpango wa kujenga skimu ya umwagiliaji Gwanumpu utakaokuwa na uwezo wa kumwagilia mashamba Ha. 170. Skimu hiyo itagharimu Tsh. 400m/= na Mradi huo utagharimiwa na Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.
Aidha wilaya ina mabwawa ya maji mawili yaliyojengwa katika vijiji vya Itumbiko na Kasuga. Upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bwawa la Cheraburo katika kijiji cha Muganza imekamilika.
Jedwali Na: 7. Miundombinu ya umwagiliaji katika Wilaya ya Kakonko 2014/15
Na |
Jina la Mradi |
Idadi ya Wakulima |
Eneo lililopimwa |
Eneo linalolimwa |
Msimu Mradi ulipoanza |
Maelezo ya ziada |
1
|
Bugunga “A”
(Muhwazi) |
278 |
Ha 150 |
Ha 202 |
2003/04 |
Uzalishaji unaendelea
|
2
|
Bugunga “B”
(Nchumito) |
250 |
Ha 138 |
Ha 128 |
2006/07 |
Uzalishaji unaendelea
|
3
|
Mwiruzi
|
180 |
Ha 152 |
Ha 140 |
2006/07
|
Uzalishaji unaendelea
|
4
|
Nyaronga
|
220 |
Ha 153 |
Ha 50 |
2008/09
|
Uzalishaji unaendelea
|
5
|
Ruhwiti
|
330 |
Ha 140 |
Ha 219 |
2004/05
|
Uzalishaji unaendelea. Ukamilishaji wa mfereji mkuu unaendelea na umefikia m. 823 kati ya lengo la m. 950.
|
6
|
Katengera
|
248 |
Ha 217 |
Ha 196 |
2006/07
|
Uzalishaji unaendelea . Usakafiaji wa mfereji mkuu unaendelea na mkandarasi anaendelea kukamilisha ujenzi wa mfereji mkuu na vigawa maji 15 mpaka kufikia Jan.2015
|
7
|
Itumbiko
[Bwawa] |
340 |
Ujazo wa Lita 28mil.
|
Matumizi ya binadamu na mifugo
|
2007/08
|
Bwawa linatumika
|
8
|
Kasuga
[Bwawa] |
210 |
Ujazo - Lt 106.5mil
|
Matumizi ya binadamu na mifugo
|
2011/12
|
Limeweka maji kidogo msimu wa mwaka 2013/14
|
JUMLA
|
2,056 |
940 |
935 |
|
|
Wilaya inaendelea kutafiti na kuanzisha skimu mpya za umwagiliaji na mabwawa ili kuongeza eneo la Kilimo cha umwagiliaji. Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Umwagiliaji Kanda ya Tabora inaendelea na utayarishaji wa mradi mpya wa umwagiliaji katika kijiji cha Gwanumpu kitakachokuwa na uwezo wa kumwagilia Ha. 170. Mradi huu utagharimiwa na Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund kwaTshs. 400mil/=. Pamoja na skimu ya Gwanumpu, Ofisi ya Umwagiliaji Kanda ya Tabora imekamilisha hatua za awali za upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bwawa la Cheraburo katika kijiji cha Muganza.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa