Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imewataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi inayotekelezwa katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 ili ikamilike kabla ya mwisho wa mwezi Desemba, 2024.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Robo ya kwanza 2024/2025 siku ya pili ya ziara Novemba 14, 2024, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Mhe.Fidel Chiza Nderego amewasisitiza mafundi kuongeza kasi wakati wa utekelezaji wa miradi waliyopewa kwa kuongeza nguvu kasi ili kukamilisha miradi kwa wakati. Aidha Mwenyekiti alimwagiza Afisa Manunuzi kupeleka vifaa kwa wakati ili mafundi waweze kukamilisha miradi kwa wakati.
Vilevile Mhe.Nderego ameeleza kuwa iwapo miradi itakamilika kwa wakati itaweza kuwasaidia makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi, wagonjwa pamoja na Wananchi katika upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Amani Mtendeli, Eneo la Shamba la Miti na parachichi Mtendeli ambalo TARI watazalisha miche ya parachichi, ujenzi wa nyumba za Wakuu wa Idara, ujenzi wa vibanda katika soko kuu la Kakonko, Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji, ujenzi wa Madarasa ya awali Shule ya Msingi Itumbiko, Ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti na chumba cha kufanyia upasuaji Hospitali ya Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa